Tumesafiri salama na tupo kigoma sasa Baada ya kumaliza ligi kuu Tanzania bara na kulitwaaa taji hilo kwa kishindo na point nyingi sasa tupo KIGOMA  kwajili ya kupambana tena ili kufikia malengo katika club yetu.

Tunawaheshimu wapinzani wetu na tunaamini mchezo utakuwa mzuri na wenyewe heshima kubwa kwetu na mashabiki wa pande zote mbili nikizungumzia SIMBA SC Vs YANGA SC Tutaingia uwanjani kama mabingwa misimu 4 mfululizo na kuilinda heshima yetu sisi kama mabingwa.

Tumejiandaa vema na hatuna majeruhi hata mmoja wote tuko salama tayari  kuwakabili wapinzani wetu.
Tunaomba mjitokeze kwa wingi ili kuipa support timu yetu ili tuweze kupata mafanikio.

#SIMBA NGUVU MOJA